KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 3 (102/3)
- samche2014
- Oct 6, 2022
- 4 min read
Sehemu A: Fasihi Simulizi
Lazima (20 marks)
Sama utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Walikuja mahasidi, ah, walikuja
Nyayo zao zikirindima, ah rindima
Kwa ghamidha ya uadui, 00 uadui
Wali Wakibeba sime
Wali wakibeba mata
Wali Wakibeba mienge
ya moto kutangazia
kwao kuwasili
Walikuja kwa ndimi
zilohimili cheche
matusi kutumwaiya.
Hawakuj ua ya kwamba
mbele ya mhimili huno wetu
wao wali vipora.
Kwenye Mlima wa Sugu, walituvamia.
Aliwakabili Mbwene
Mwana wa Ngwamba, ee Mbwene
Aliwakabili Mbwene kwa kitali kikali.
Wali wametuteka ja samaki kwenye dema
Wali wamewapukutisha
wetu mabarobaro
Aliwakabili Mbwene
Ee Mbwene, Mwana Wa Ngwamba
Aliwakabili
kwa hamasa za ujana
kwa uchungu wa kuumbuliwa
wa wetu wana.
Aliwakabili Mbwene
Nao wakalipiza shambulizi
kwa kujidai majagina
walijibwaga uwanjani
Laiti wangalijua wanajikabidhi
viganjani mwa Mbwene.
Aliwakabili Mbwene, ee
Mwana wa Ngwamba, shujaa asoshindwa
alipigana kitali
cha kufa na kupona
kuiopoa jamii yetu,
kuirejesha hadhi yetu.
kuirejesha mifugo yetu
kuwarejeshea wakulima vikataa vyao
kuwaokoa vipusa wetu
nyara Waliotekwa, ati Walipiza kisasi.
Aliwakabili Mwana Wa Ngwamba
Aliwakabili Upepo Wa Kusi
Hata kikorno cha mapambano kilipofika
Wagundi walijua kwamba
Walikuwa na Mwana, ee Mwana
Mbwene, ee Mwana wa Ngwamba Hakuwa na kifani, ee kifani
Alipigana nao, cc Mwana wa N gwamba
Kwa siku kumi bila tonge wala tone la maji
Kwetu kukenda kicheko cha Wokovu
Kwao kukenda kilio.
(a) “Huu ni wimbo wa sifa.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mitatu kutoka kwenye utungo huu. (alama 3)
(b) Andika sifa tatu za jamii ya nafsineni katika utungo huu. (alama 3)
(c) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vinane vya kimtindo ambapo nafsineni imetumiwa kufanikisha uwasilishaji wa umngo huu. (alama 8)
(d) Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii yako. Fafanua hoja sita utakazotumia kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii. (alama 6)
SEHEMU B: RIWAYA K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea Jibu swali la 2 au la 3.
2. “Lakjni waliogopamwaliogopa hata kuwa na uoga.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Bainisha tamathali lnoja ya usemi ambayo imetumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
(c) Kwa kurejelea hoja kumi na nne kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba raia wa Tornoko walistahili kuogopa hata kuwa na uoga‘ (alama 14)
3. (a) “Usinivue nguo kwa macho yako wee!”
Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenyc riwaya hii, thibitisha kwamba mzungumzaji anastahili kuvuliwa nguo. (alama 12)
(b) Tathmini umuhimu wa barua ya Ben Bella kwa Mashaka katika kuijenga riwaya hii. (alama 8)
SEHEMU C: TAMTHILIA T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5.
4. “Tuyashughulikie ya leo. Kesho, keshokutwa na mtondo harutakuwepo. Wayatakig nigi ya mtongggoo? "
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Bainisha sifa ya rnzungumzaji inayodokezwa na kauli iliyopigiwa mstari. (alama 1)
(c) Eleza sifa tano Za anayeambiwa maneno haya. (alama 5)
(d) Kwa kurejelea hoja kumi kutoka kwenye tamthilia, onyesha jillsi kutoyataka ya mtondogoo kulivyozorotesha hali ya maisha Cheneo. (alama 10)
5. “Ni mgao Wa wakubwa kula kwanza na sisi wengine kupigania makombo yanayoanguka chini.” (a) Fafanua sifa tano za rnzungumzaji. (alama 5)
(b) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hoja kumi na tano kutoka kwenye tamthilia. (alama 15)
SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7.
6. Soma shairi lzfuatalo kisha ujibu maswali.
Mwanangu, Wenye dhambi vishawishi, vikejeli
Mwanangu, katu wasikushawishi, binkuli
Mwanangu, aushi nayo uishi, kama mwali
Mwanangu sikubali!
Mwanangu, sherati sikuperembc, kakubali
Mwanangu, usiwache wakubembe, kwa sali,
Mwanangu, mithili yao mapembe, ya fahali
Mwanangu sikubali!
Mwanangu, wajeuri siwe nao, ni shubili
Mwanangu usifwate njia zao, pita mbali
Mwanangu, ujeuri scra yao, mazohali,
Mwanangu sikubali!
Mwanangu, Waongo usiwasifu, kulihali
Mwanangu, uongo ubatilifu, si amali
Mwanangu, ndimi zao hazikifu, si manzili
Mwanangu sikubali!
Mwanangu, wafisadi siwe nao, kemikali
Mwanangu, tamaa ndo utu wao, si Injili
Mwanangu, Wahepe kila uchao, kiakili
Mwanangu sikubali!
Mwanangu, wote walio wabaya, Wanadhili
Mwanangu, usije ukawapeya, ikibali
Mwanangu, katika hino duniya, kaa mbali
Mwanangu sikubali!
(J. Kiponda)
( a) Fafanua mambo sita ambayo yanaweza kuzorotesha maadili ya anayelengwa na shairi hili.
(b) Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.
(c) Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shain' hili.
(d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyoz
(i) idadi ya vipande katika mishororo.
(ii) mpangilio wa maneno katika mishororo
(m) idadi ya mizani katika mishororo.
(iv) mpangilio wa vina katika beti.
(e) Andika aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika shairi hili.
if I Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari.
Soma Shairi Iifizatalo kisha ujibu maswali.
Walo nacho hawachi
mshangao kunitia
Moyoni watakutia
pindi waonapo
we u chambo cha
kuvutia rasilimali
huko kwenye vina
Hawachi
kukwinamisha
kukupindisha mgongo
ndoana urneshika
kuvulia yao riziki.
Watakwita kwa majina
ya hadhi ya kupembeja
ya kukwaminisha
kwamba We na wao mu
Wamoja
hali zenu
kama sahani na kawa
wanakwonyesha wao
nawe
mwachumia jungu moja
yenu matarajio ni mamoja
Watakwahidi halua
kila tunu watakwashiria
mradi nyoyo zao zimemaizi
We u nundu
ya kukamulia mafuta
we u ndovu
wa mti kugonga
makoma kuangusha
wafaidi wao.
Mabepari wana mambo
ukiwa yao makasia
ya kuliendesha dau lao
majini lielee
miamba kulepusha
Watakusifil
Watakuchajiisha
mbele utunge
machoyo yenye ari
huku wanakufunga nira
ja fahali
mali kuwazalishia
huku kipato wakupimia
kwa kibaba
usipate kukidhi haja
usipate kujarnini
kuwategemea uzidi.
Hawa ni wa kuajabiwa
Watakupa yao kazi
Mpangilio wa kazi
wakukabidhi Wao
na malengo wakupe
La! Hawakupi!
Wanakuhusisha
katika kuyavyaza na
muda wa kuyafikia
nao mwaafikiana
ati kuna makubaliano bayana
ambayo ubatizo Wayo ni
kandarasi ya utcndakazi.
Ela We nao mnajua
ndo kigezo cha kupimia
Wako uwaj ibikaji
wako mchango chunguni
yako thamani
Na usidhani una hiari ya
kuamua tapofika
Watakusukuma
lmfikia yao shabaha
bila lmwazia
ujixa wanokupa.
Watakuhimiza
kuturnia chako kipawa
kuikoza nundu yao mafuta
Viumbe hawa!
Mabepari - waajiri
(a) Eleza mikakati sita inayotumiwa na waajiri kujikuza kiuchumi. (alama 6)
(b) Bainisha tamathali tatu za usemi zilizoturniwa katika shairi hili. (alama 3)
(c) Huku ukitoa mifano, bainisha aina mbili za uhum wa kishairi aliotumia mshairi.
(d) Andika mifano ya mistari mishata katika shairi hili.
(6) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
SEHEMU E: HADITH FUPI K. Walibora na S. A. Mohamed (Wah): Damu Mveusi na Hadithi Nyingine
8. (a) Tathmini urnuhimu wa Lucy katika kuijenga hadithi, “Tazamana na mauti"
“Mizizi ya Matawi” (Ali A. Ali)
(b) “Aaa, bibi yangu namuomba Mungu anisamehe dhambi zangu .."’
(i) Eleza muktadha Wa dondoo hili.
(ii) “Jamii ya,” Mizizi ya Matawi azamana na Mauti.”atawi inastahili kusamehewa ” Fafanua kwa kutoa hoja sita kutoka kwenye hadithi.




Comments